1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti
  3. Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Hadithi Macho ya aina mbili hautoyagusa moto: Jicho lililolia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu, na jicho lililokesha likilinda kwaajili ya Mwenyezi Mungu

عن ابن عباس رضي الله عنهما مرفوعاً: «عَيْنَانِ لاَ تَمسُّهُمَا النَّار: عَيْنٌ بَكَتْ من خَشْيَة الله، وعَيْنٌ بَاتَت تَحْرُسُ في سَبِيل الله».

Kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Macho ya aina mbili hautoyagusa moto: Jicho lililolia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu, na jicho lililokesha likilinda kwaajili ya Mwenyezi Mungu".

Sahihi Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy

Ufafanuzi

Maana ya hadithi: Nikuwa moto hautogusa jicho lililolia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo pindi anapokumbuka mtu ukubwa wa Mwenyezi Mungu na uwezo wake juu ya waja wake na uzembe wake katika haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu; akalia kwa kutaraji rehema zake na kuogopa adhabu zake na hasira zake, basi huyu kaahidiwa kusalimika na moto. Na jicho jingine ambalo moto hautoligusa, nalo ni: Yule atakayelala akilinda kwaajili ya Mwenyezi Mungu katika mipaka au sehemu ya mapigano kwa kuhifadhi roho za waislamu. Na kauli yake: "Hautoyagusa moto" Hii ni katika sehemu ya kutaja sehemu ya kitu na makusudio yake ni chote: nakuwa atakayelia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu na atakayelala akilinda katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu anaiharamisha miili yao katika moto.

Kuonyesha Tafsiri

18 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية