1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti
  3. Akida- Itikadi-

Hadithi Alifariki Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- hali yakuwa hakuna chochote nyumbani kwake anachoweza kukila mwenye ini (uhai) ila kiasi kidogo cha ngano kilichokuwa katika ubao wangu (wa kuhifadhia chakula), nikala mpaka kikakaa muda mrefu, nilipokipima kikamalizika

عن عائشة رضي الله عنها قالت: تُوُفِّيَ رسول الله صلى الله عليه وسلم وما في بيتي من شيء يَأكُلُهُ ذُو كَبدٍ إلا شَطْرُ شَعير في رَفٍّ لي، فأكَلتُ منه حتى طال عليَّ، فَكِلْتُهُ فَفَنِيَ.

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Alifariki Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- hali yakuwa hakuna chochote nyumbani kwake anachoweza kukila mwenye ini (uhai) ila kiasi kidogo cha ngano kilichokuwa katika ubao wangu (wa kuhifadhia chakula), nikala mpaka kikakaa muda mrefu, nilipokipima kikamalizika

Sahihi Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Anaeleza Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alifariki hali yakuwa hakuna nyumbani kwake chochote isipokuwa kiasi kidogo cha ngano, na maana yake ni kiwango kidogo cha ngano, kama alivyoifasiri imamu Tirmidhiy, akaendelea kula katika chakula alichokiacha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa muda mrefu, alipokipima kikamalizika, na hii ni ishara ya kuendelea kwa baraka zake -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika chakula hicho kidogo, pamoja na kutokuwepo kwa kipimo kinachoonyesha kiasi wakati wa kumtegemea Mwenyezi Mungu, kipimo wakati wa kuuziana kinahitajika kwaajili ya kuweka sawa haki ya wale wenye kuuziana, ama kipimo wakati wa kutoa sadaka haipendezi (si katika sunna).

Kuonyesha Tafsiri

18 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية