1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti
  3. Akida- Itikadi-

Hadithi Kwani hawaharamishi aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayaharamisha? na wanahalalisha aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayahalalisha? Nikasema: Ndivyo, Akasema: Basi huko ndiko kuwaabudu.

عن عدي بن حاتم رضي الله عنه : "أنه سمع النبي صلى الله عليه وسلم يقرأ هذه الآية: "اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِنْ دُونِ اللَّهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُوا إِلاَّ لِيَعْبُدُوا إِلَهًا وَاحِدًا لا إِلَهَ إِلاَّ هُوَ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ" فقلت له: إنا لسنا نعبدهم، قال: أليس يُحَرِّمُونَ ما أحل الله فتُحَرِّمُونَهُ؟ ويُحِلُّونَ ما حَرَّمَ الله فتُحِلُّونَهُ؟ فقلت: بلى، قال: فتلك عبادتهم".

Kutoka kwa Adiy bin Hatim-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alimsikia Mtume rehema na Amani ziwe juu yake Akisoma aya hii: "Wamewafanya wanachuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu kinyume na Mwenyezi Mungu na Masihi mwana wa Mariam, na hawakuamrishwa ila ni kumuabudu Mungu mmoja, hapana Mola ispokuwa yeye, ametakasika na yale wanayomshirikisha nayo" Nikasema kumwambia: Hakika sisi hatuwaabudu wao, Akasema: "Kwani hawaharamishi aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayaharamisha? na wanahalalisha aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayahalalisha? Nikasema: Ndivyo, Akasema: Basi huko ndiko kuwaabudu".

Sahihi Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy

Ufafanuzi

Aliposikia swahaba huyu mtukufu kisomo cha Mtume rehema na Amani zimfikie cha Aya hii ambayo ndani yake kuna habari kwa Mayahudi na wakristo: kuwa wao wamewafanya wanachuoni wao na wachamungu wao kuwa miungu, wanawawekea sheria zinazokwenda kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu na wakawatii juu ya hilo, ikamtatiza maana yake, kwasababu yeye alikuwa akidhania kuwa ibada inaishia katika kusujudu na mfano wake, Mtume rehema na Amani zimfikie akambainishia- kuwa katika kuwaabudu wanachuoni na watawa: ni kuwatii katika kuhalalisha haramu na kuharamisha halali, kinyume na hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake rehema na Amani zimfikie.

Katika Faida za Hadithi

  1. Nikuwa kuwatii wanachuoni na wengineo katika viumbe katika kubadili hukumu za Mwenyezi Mungu-ikiwa mwenye kuwatii anajua kuwa huko ni kwenda kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu- ni shirki kubwa.
  2. Nikuwa kuhalalisha na kuharamisha ni haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  3. Kubainishwa kwa aina miongoni mwa aina za shirki, nayo ni shirki ya kutii.
  4. Sheria ya kumfundisha mjinga.
  5. Nikuwa maana ya ibada ni pana, inakusanya yote anayoyapenda Mwenyezi Mungu na kuyaridhia katika maneno na matendo ya wazi na ya siri.
  6. Kubainishwa upotofu wa wanachuoni na watawa.
  7. Kuthibitishwa kwa ushirikina wa Mayahudi na Wakristo.
  8. Nikuwa, asili ya dini ya Mitume ni moja, nayo ni Tauhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu).
  9. Nikuwa kumtii kiumbe katika kumuasi muumba nikumuabudu.
  10. Ulazima wa kutaka ufafanuzi kutoka kwa wenye elimu kwa yale ambayo hukumu yake imefichikana.
  11. Pupa ya maswahaba juu ya elimu.

Kuonyesha Tafsiri

28 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
DE Deutsch الألمانية
JA 日本語 اليابانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
Aina tofauti tofauti