1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti
  3. Fiq'hi na misingi yake.

Hadithi Tulikuwa tukimuandalia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- mswaki wake na (maji yake kwaajili ya) twahara, basi Mwenyezi Mungu anamuamsha kwa muda anaotaka aamke nyakati za usiku, anapiga mswaki, na anatawadha na anaswali

عن عائشة رضي الله عنها ، قالت: كُنَّا نُعِدُّ لرسول الله صلى الله عليه وسلم سِوَاكَهُ وَطَهُورَهُ، فَيَبْعَثُهُ الله ما شاء أن يَبْعَثَهُ من الليل، فَيَتَسَوَّكُ، ويتوضَّأ ويُصلي.

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Tulikuwa tukimuandalia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- mswaki wake na (maji yake kwaajili ya) twahara, basi Mwenyezi Mungu anamuamsha kwa muda anaotaka aamke nyakati za usiku, anapiga mswaki, na anatawadha na anaswali

Sahihi Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Anaeleza Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa yeye alikuwa akimuandalia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- mswaki wake, na maji ambayo atayatumia kutawadha usiku, kisha anamuamsha Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka nyakati za usiku, wakati wowote usiku, anapoamka tu anaanza kusugua meno yake kwa mswaki; ili aondoe harufu ya mdomo ambayo hutokea mara nyingi kwasababu ya kulala, kisha anatawadha udhu wake wa swala, kisha anaswali swala za usiku.

Kuonyesha Tafsiri

17 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية