1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti
  3. Fiq'hi na misingi yake.

Hadithi Atakayeswali swala ya Asubuhi basi huyo yuko katika dhima ya Mwenyezi Mungu

عن جُندب بن عبد الله القَسْرِِي رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«مَنْ صَلَّى صَلَاةَ الصُّبْحِ فَهُوَ فِي ذِمَّةِ اللهِ، فَلَا يَطْلُبَنَّكُمُ اللهُ مِنْ ذِمَّتِهِ بِشَيْءٍ، فَإِنَّهُ مَنْ يَطْلُبْهُ مِنْ ذِمَّتِهِ بِشَيْءٍ يُدْرِكْهُ، ثُمَّ يَكُبَّهُ عَلَى وَجْهِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ».

Kutoka kwa Jundub bin Abdillah Al-Kasri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakayeswali swala ya Asubuhi basi huyo yuko katika dhima ya Mwenyezi Mungu, basi asikukoseni Mwenyezi Mungu kwa chochote katika dhima yake, na atakayetafutwa na Mwenyezi Mungu katika dhima yake kwa chochote humdiriki (humuadhibu), kisha humburuza kwa uso wake motoni".

Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim Swahiih Muslim - 657

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwenye kusali Al-Fajiri basi huwa katika hifadhi ya Mwenyezi Mungu na ulinzi wake na himaya yake, akimtetea, na akimnusuru.
Kisha akatahadharisha -Rehema na amani ziwe juu yake- kutoivunja ahadi hii na kuiharibu, ima kwa kuiacha swala ya Al-fajiri, au kumkwaza mwenye kuisali na kumfanyia uadui, kwani mwenye kufanya hivyo atakuwa kauharibu ujirani huu, na atakuwa amestahiki ahadi hii kali, kwa Mwenyezi Mungu kumchunguza yale aliyoyapuuza katika haki zake, na mwenye kuchunguzwa na Mwenyezi Mungu humtia hatiani, kisha humtupa kwa uso wake katika moto.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa umuhimu wa swala ya Alfajiri na fadhila zake.
  2. Tahadhari kubwa ya kumsumbua kwa ubaya aliyesali Alfajiri.
  3. Allah huwalipiza kisasi wenye kuwasumbua waja wake wema.

Kuonyesha Tafsiri

68 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
JA 日本語 اليابانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
KY Кыргызча القيرقيزية
NE नेपाली النيبالية
YO Yorùbá اليوروبا
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
SO Soomaali الصومالية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
CS Čeština التشيكية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
FF Fulfulde الفولانية
IT Italiano الإيطالية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
BG Български البلغارية
AZ Azərbaycan الأذربيجانية
EL Ελληνικά اليونانية
AK Akan الأكانية
UZ O‘zbek الأوزبكية
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
LN Lingala اللينجالا
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
BM Bambara البامبارية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية
RN Kirundi الكيروندي
YAO Yao الياو
KMR Kurmancî الكرمنجية