عَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ رَضيَ اللهُ عنها أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«لَا تُحِدُّ امْرَأَةٌ عَلَى مَيِّتٍ فَوْقَ ثَلَاثٍ إِلَّا عَلَى زَوْجٍ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا، وَلَا تَلْبَسُ ثَوْبًا مَصْبُوغًا إِلَّا ثَوْبَ عَصْبٍ، وَلَا تَكْتَحِلُ، وَلَا تَمَسُّ طِيبًا إِلَّا إِذَا طَهُرَتْ نُبْذَةً مِنْ قُسْطٍ أَوْ أَظْفَارٍ».
المزيد
Imepokelewa kutoka kwa Ummu Atwiya -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Asiache mapambo na kupendeza mwanamke yeyote kwa maiti zaidi ya siku tatu, isipokuwa kwa mume wake atakaa miezi minne na siku kumi, na wala asivae nguo yenye urembo isipokuwa nguo yenye urembo kiasi, wala asipake wanja, wala asiguse manukato, isipokuwa atakapotwaharika anaweza kuchukua kiasi kidogo cha Qustwi au Adhfar (aina ya marashi ya kufukiza, hutumiwa na wanawake)".