1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti
  3. Fiq'hi na misingi yake.

Hadithi Anachokipata aliyekufa shahidi katika maumivu ya kifo, ni kama maumivu anayoyapata mmoja wenu kutokana na kung'atwa na mdudu chungu

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «مَا يَجِدُ الشَّهيد من مَسِّ القتل إلا كما يَجِدُ أَحَدُكُمْ من مَسِّ القَرْصَةِ».

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Anachokipata aliyekufa shahidi katika maumivu ya kifo, ni kama maumivu anayoyapata mmoja wenu kutokana na kung'atwa na mdudu chungu".

Ni nzuri Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na An-Nasaaiy - Imepokelewa na Ahmad - Imepokelewa na Addaaramy

Ufafanuzi

Maana ya hadithi: nikuwa mtu atakapokufa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hakika yale yanayompata katika mguso wa kifo, na katika riwaya ya Daaramiy (katika maumivu ya kifo) hayahisi isipokuwa ni kama anavyohisi mmoja wetu anapong'atwa na mdudu chungu, na katika riwaya ya Daaramiy "kutokana na maumivu ya kung'atwa". Na maana yake nikuwa: Shahidi hasongwi na ukali wa maumivu ya kifo, kama ilivyo hali ya watu wengine, bali ukali anaoupata na ukamsumbua wakati wa kifo chake ni kama ule tunaoupata kwasababu ya kung'atwa na mdudu chungu, na maumivu anayosababu mdudu huyo na uharaka wa kumalizika kwake, basi wala hayahisi, Na hii ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa shahidi, kwani yeye alipoitanguliza roho yake katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kiurahisi, basi Mwenyezi Mungu akampunguzia juu yake maumivu ya kuuwawa.

Kuonyesha Tafsiri

18 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية