1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti
  3. Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Hadithi Hakuna watu wowote watasimama katika kikao ambacho hawamtaji Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, isipokuwa watanyanyuka mithili ya mzoga wa punda, na wanakua na majuto

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَا مِنْ قَوْمٍ يَقُومُونَ مِنْ مَجْلِسٍ لَا يَذْكُرُونَ اللَّهَ فِيهِ إِلَّا قَامُوا عَنْ مِثْلِ جِيفَةِ حِمَارٍ، وَكَانَ لَهُمْ حَسْرَةً».

Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hakuna watu wowote watasimama katika kikao ambacho hawamtaji Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, isipokuwa watanyanyuka mithili ya mzoga wa punda, na wanakua na majuto".

Sahihi Imepokelewa na Abu Daud Sunanu Abii Daud - 4855

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba hakuna kundi la watu watakaokaa katika kikao kisha wakanyanyuka katika kikao hicho haliyakuwa hawajamtaja Mwenyezi Mungu ndani yake isipokuwa watanyanyuka katika mfano wa mzoga wa punda katika kunuka na uchafu; na hii ni kwa sababu walishughulika na mazungumzo wakaacha kumtaja Mwenyezi Mungu, na kikao hicho kwao kitakuwa ni masikitiko siku ya Kiyama na ni mapungufu na majuto kwao.

Katika Faida za Hadithi

  1. Yaliyotajwa katika kutahadharisha kughafilika na kumtaja Mwenyezi Mungu hayaishii katika kikao pekee, bali yanaenea mahala pengine, amesema Imam Nawawi: Ni machukizo kwa atakayekaa mahali aondoke kabla hajamtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake.
  2. Masikitiko yatakayotokea kwao siku ya Kiyama: Ima kwa kupitwa na malipo na thawabu kwa kutofaidika na wakati katika kumtii Mwenyezi Mungu, na ima kwa madhambi na adhabu kwa kuutumia wakati kwa kumuasi Mwenyezi Mungu.
  3. Tahadhari hii ni pale kujisahau kutakapokuwa ni kwa mambo ya halali, vipi kwa vikao vya haramu ambavyo ndani yake kuna utesi na usengenyaji na mengineyo?!.

Kuonyesha Tafsiri

51 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
NE नेपाली النيبالية
YO Yorùbá اليوروبا
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية