1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti
  3. Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Hadithi Nilionyeshwa Pepo na Moto, katu sijawahi kuona katika kheri na shari mfano wa siku hiyo, na lau mngejua ninayoyajua basi mngelicheka kidogo na mngelia sana

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: بَلَغَ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ‌عَنْ ‌أَصْحَابِهِ ‌شَيْءٌ، فَخَطَبَ فَقَالَ:
«عُرِضَتْ عَلَيَّ الْجَنَّةُ وَالنَّارُ فَلَمْ أَرَ كَالْيَوْمِ فِي الْخَيْرِ وَالشَّرِّ، وَلَوْ تَعْلَمُونَ مَا أَعْلَمُ لَضَحِكْتُمْ قَلِيلًا وَلَبَكَيْتُمْ كَثِيرًا» قَالَ: فَمَا أَتَى عَلَى أَصْحَابِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَوْمٌ أَشَدُّ مِنْهُ، قَالَ: غَطَّوْا رُءُوسَهُمْ وَلَهُمْ خَنِينٌ، قَالَ: فَقَامَ عُمَرُ فَقَالَ: رَضِينَا بِاللهِ رَبًّا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، وَبِمُحَمَّدٍ نَبِيًّا، قَالَ: فَقَامَ ذَاكَ الرَّجُلُ فَقَالَ: مَنْ أَبِي؟ قَالَ: «أَبُوكَ فُلَانٌ»، فَنَزَلَتْ: {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِنْ تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ} [المائدة: 101].

Kutoka kwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Lilimfikia jambo Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Maswahaba zake, akawahutubia akasema:
"Nilionyeshwa Pepo na Moto, katu sijawahi kuona katika kheri na shari mfano wa siku hiyo, na lau mngejua ninayoyajua basi mngelicheka kidogo na mngelia sana" Akasema: Haikuwahi kutokea kwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ngumu kama hiyo, akasema: Wakafunika nyuso zao huku wakitoa sauti za kugugumia (kwa vilio), anasema: Akasimama Omari akasema: Tumemridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na Uislamu kuwa dini, na Muhammadi kuwa Nabii, anasema: akasimama yule bwana akasema: Ni nani baba yangu? Akasema: "Baba yako ni fulani", ikateremka: "Enyi mlioamini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni" [Al-Maaida: 101].

Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Swahiih Muslim - 2359

Ufafanuzi

Lilimfikia jambo Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Maswahaba zake, nalo ni kwamba wao walimzidishia maswali, akakasirika, na akawahutubia, akasema: Nimeonyeshwa Pepo na Moto; sikuwahi kuona kheri nyingi kuliko nilizoziona siku ya leo Peponi, wala shari kubwa kuliko nilizoziona siku hiyo Motoni, na lau kama mngeliona nilichokiona, na mkajua ninachokijua katika yale niliyoyaona siku ya leo na kabla ya leo, basi mngelihuzunika huzuni kubwa, na kungepungua kucheka kwenu, na kungezidi kulia kwenu. Anasema Anasi radhi za Allah ziwe juu yake: Haikuwahi kutoka kwa Maswahaba wake rehema na amani ziwe juu yake siku ngumu kama hiyo, na wakafunika vichwa vyao huku wakitoa sauti ya kunung'unika inayotoka puani kwa sababu ya kulia sana. Akasimama Omari radhi za Allah ziwe juu yake akasema: Tumemridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na Uislamu kuwa dini, na Muhammadi kuwa Nabii. Akasema: Akasimama yule bwana, akasema: Nani baba yangu?
Akasema: "Baba yako ni fulani", ikateremka: "Enyi mlioamini! Msiulize kuhusu mambo ambayo yakikudhihirikieni yatakuchukizeni" [Al-Ma’idah: 101].

Katika Faida za Hadithi

  1. Ni Sunna kulia kwa kuhofia adhabu ya Mwenyezi Mungu, na kutokithirisha kucheka; kwa sababu hilo linaonyesha kughafilika na ugumu wa moyo.
  2. Waliathirika na mawaidha Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, na hofu yao kubwa dhidi ya adhabu za Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
  3. Sunna ya kufunika uso wakati wa kulia.
  4. Amesema Al-Khattwabi: Hadithi hii ni kwa mtu aliyeuliza kwa kuchokonoa mambo au kwa ukaidi katika mambo ambayo hana haja nayo, ama atakayeuliza kwa dharura, kwa kutokewa na jambo akaliulizia, huyu hana dhambi juu yake wala lawama.
  5. Himizo la kuwa na msimamo katika kumtii Allah, na kujitenga mbali na kumuasi Allah, na kusimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu.
  6. Hapa inaonyesha kufaa kukasirika wakati wa mawaidha na wakati wa kufundisha.

Kuonyesha Tafsiri

40 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
MOS Moore الموري
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية