1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti
  3. Fiq'hi na misingi yake.

Hadithi Fuatanisheni kati ya Hija na Umra, kwani huondoa umasikini na madhambi kama moto unavyoondoa uchafu wa chuma, na dhahabu, na fedha, na haina Hija nzuri na safi malipo isipokuwa Pepo

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«تَابِعُوا بَيْنَ الحَجِّ وَالعُمْرَةِ، فَإِنَّهُمَا يَنْفِيَانِ الفَقْرَ وَالذُّنُوبَ كَمَا يَنْفِي الكِيرُ خَبَثَ الحَدِيدِ، وَالذَّهَبِ، وَالفِضَّةِ، وَلَيْسَ لِلْحَجَّةِ الْمَبْرُورَةِ ثَوَابٌ إِلاَّ الجَنَّةُ».

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Fuatanisheni kati ya Hija na Umra, kwani huondoa umasikini na madhambi kama moto unavyoondoa uchafu wa chuma, na dhahabu, na fedha, na haina Hija nzuri na safi malipo isipokuwa Pepo".

Sahihi Imepokelewa naTirmidhiy na Nasai na Ahmad Sunanu Tirmidhiy - 810

Ufafanuzi

Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuweka karibu kati ya kutimiza ibada ya Hija na ibada ya Umra, na kutoacha kuzitekeleza hali yakuwa kuna uwezo, kwa sababu kuzitekeleza kwake inakuwa ni sababu ya kuondoa umasikini na madhambi na athari zake ndani ya moyo, kama ambavyo mpulizo wa moto huwa sababu ya kuondoa uchafu wa chuma na vyote vinavyochanganyika nacho katika madini ambayo si chuma.

Katika Faida za Hadithi

  1. Fadhila za kufuatanisha baina ya Hija na umra na himizo katika hilo.
  2. Kufuatanisha kati ya Hija na Umra ni miongoni mwa sababu za utajiri na msamaha wa madhambi.
  3. Amesema Al-Mubaarakafuriy: (Huondoa umasikini) Yaani: Huuondosha kabisa, na hii inategemea maana zote mbili: Umasikini unaoonekana kwa kupatikana utajiri wa mkononi, na umasikini wa ndani, kwa kupata utajiri wa moyo.

Kuonyesha Tafsiri

34 Lugha
EN English الإنجليزية
ID Indonesia الإندونيسية
BN বাংলা البنغالية
TR Türkçe التركية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
MOS Moore الموري
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية