عَنْ أَبِي طَلْحَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«لاَ تَدْخُلُ المَلاَئِكَةُ بَيْتًا فِيهِ كَلْبٌ وَلاَ صُورَةٌ».

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Hawaingii Malaika nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha"

Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Swahiih Al Bukhaariy - 3322

Ufafanuzi

Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika wa rehema hawaingii nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha za viumbe hai; Hii ni kwa sababu sura ya kitu ambacho kina roho ni dhambi kubwa, na kuna uigaji wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu, na ni njia katika njia za ushirikina, na baadhi yake ni picha ya vile vinavyoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu. Ama sababu ya kujiepusha na nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa; ni kwa sababu anakula uchafu mwingi, na ni kwa sababu baadhi mbwa huitwa mashetani; Na malaika wako dhidi ya mashetani. Na kwa sababu ya harufu mbaya ya mbwa; Malaika wanachukia harufu mbaya, na kwa sababu ni haramu kuwafuga; Hivyo mwenye kuwafuga akaadhibiwa kwa kunyimwa Malaika kuingia nyumbani kwake, na kuswali humo, na kumuombea msamaha, kumbariki yeye na nyumba yake, na kumzuilia udhia wa Shetani.

Katika Faida za Hadithi

  1. Uharamu wa kufuga mbwa isipokuwa mbwa wa mawindo au mifugo au mazao.
  2. Kuwa na picha ni miongoni mwa mambo maovu ambayo Malaika huchukizwa nayo, na kuwepo kwake mahali hapo ni sababu ya kunyimwa huruma, na hivyo hivyo kwa mbwa.
  3. Malaika ambao hawaingii ndani ya nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha ni Malaika wa rehema, lakini kwa walinzi na wengine ambao wana kazi kama Malaika wa mauti, wanaingia kila nyumba.
  4. Uharamu wa kutundika picha za viumbe wenye roho juu ya kuta na kwingineko.
  5. Amesema Al-Khattwabi: Bali Malaika hawaingii ndani ya nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha, jambo linalopelekea uharamu wa kumiliki mbwa na picha, ama mbwa wasiokuwa haramu ni kama vile mbwa wa kuwinda, wa mazao, na wa mifugo, na picha zinazotumika katika zulia, mito, na vitu vingine, kwa kukanyagwa na kudhalilishwa hizi haziwezi kuwa sababu ya kuzuia Malaika kuingia.

Kuonyesha Tafsiri

53 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
KY Кыргызча القيرقيزية
NE नेपाली النيبالية
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
CS Čeština التشيكية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
AZ Azərbaycan الأذربيجانية
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية